wafanya biashara wadogo wadogo wa chakula maarufu mama rishe wa eneo la kwa morombo wamewaomba wateja wao kuwa wastaarabu pindi wanapotumia huduma zao
Hayo yamemwa na baadhi ya wafanya biashara walipokuwa wakihojiwa kwa nyakati tofauti na mmoja wa waandishi wa habari wa ajtc
Bi Fatma Ally ambaye ni mmoja wa mama lishe hao amesema katika biashara hiyo wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ikiwemo na wateja kula chakula bila kulipa na kutoridhika na kipimo wanachopimiwa na mama lishe hao
Ameendelea kusema kuwa wateja hao ambao wengi ni wafanya kazi kutoka makampuni mbalimbali wamekuwa wakimwaga vyakula chini wakati wa kula na kusababisha uchafu katika eneo hilo
Pamoja na hayo Bi Susan Mabula ambae pia ni mmoja wa mama lishe hao hakusita kuelezea hasara wanayo ipata katika biashara hiyo ikiwemo na wateja hao kukopa chakula na kuchelewa kurejesha fedha hivyo kusababisha mama lishe hao kushindwa kununua bidhaa kama mchele na unga
Naye mmoja wa wafanya kazi hao ambaye ni mfanya kazi wa kampuni ya B AND B GEMS inayojishughulisha na madini Bw Heluman Amos amesema kuwa sio wote ambao wana tabia hiyo ila wapo wnye tabia kama hizo
Sanjari na hayo Bi Susan Mabula amemalizia kwa kusema anawashauri wakina mama wenzake kuwa na umoja katika yao