AJTC NEWS

Friday, March 28, 2014

ROSE NDAUKA ADAIWA KUMTIBULIA DILI BATULI

Stori:Hamida Hassan na Gladness Mallya
Mastaa wawili, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ na Rose Ndauka wamedaiwa kuwa kwenye bifu chanzo kikidaiwa ni Rose kumtibulia mwenzake dili la ile project ya kusafisha jiji iliyofanyika hivi karibuni.
Malkia wa filamu za kibongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
Akizungumza na Ijumaa kwa sharti la kutotajwa jina lake, chanzo kilisema, wazo la project ile alikuwa nalo Batuli lakini Rose akaingilia kati, hali iliyosababisha....

DIAMOND ACHEFUA WAISLAM

Stori: Hamida Hassan na Shakor Jongo
KIJOGOO wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewachefua waumini wenzake wa Kiislamu baada ya kutupia swaga za staili ya Ngololo kwenye shughuli ya Maulidi.
Kijogoo wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz akicheza staili ya Ngololo kwenye kaswida.
Tukio hilo lililowagusa waumini hao lilitokea juzikati ambapo kulifanyika Maulidi ya kumtoa nje mtoto wa dansa wake aitwaye Moze Lyobo maeneo ya Mbagala, jijini Dar.
Awali watu waliokuwepo eneo hilo walifurahia uwepo wake lakini.........

MMJKT MABINGWA WA NGUMI MKOA WA DAR ES SALAAM

Bondia Hamisi Mputeni kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Victor Njaiti wakati wa mpambano wao katika mashindano ya klabu bingwa mkoa wa Dar es salaam juzi Njaiti alishinda kwa pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mohamed Chibumbuli kushoto akionyeshana umwamba wa kutupiana makonde na Abdul Rashid wakati wa mchezo wao katika mashindano ya klabu bingwa mkoa wa Dar es salaam Chibumbuli alishinda kwa pointi katika mchezo huo juzi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
……………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya MMJKT jana imeibuka mabigwa wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam baada ya kuvipiku vilabu nane vilivyoweza kujitokeza kushiliki mashindano hayo na kutawazwa kuwa bingwa wa mkoa, baadhi ya mabondia waliocheza fainali za mashindano hayo ni Hamisi Mrisho wa ‘MMJKT’ alisambalatishwa kwa pointi na bondia Oscar Richard wa ‘Urafiki’ na Omari Mohamed wa urafiki akichezea kichapo kutoka kwa mwenzie John Mwambinga, na bondia anayekuja kwa kasi ya hali ya juu akitokea timu ya Ashanti ya ilala kwa sasa akichezea timu ya ‘MMJKT’ alifanikiwa kumpiga John Christian wa ‘Mgulani’ Saleh Abdallah wa mgulani alishindwa kutamba mbele ya Undule Langson wa Magereza
Nae Jacobo Agusteno wa ‘Mgulani’ alishindwa kufurukuta mbele ya Bosco Bakari wa ‘MMJKT’ katika mpambano mwingine uliowakutaniasha Festo Ngabo wa Magereza alishindwa kutamba mbele ya Victor Njaiti wa ‘MMJKT’ nae bondia Mohamedi Chibumbuli wa magereza alimsambaratisha vibaya bondia Said Saleh wa ‘mavituzi’
Akizungumzia maandalizi ya mabondia wa mkoa wa Mwenyekiti wa chama cha ngumi mkoa wa Dar es salaam ‘DABA’ Akaroli Godfrey amesema kwa sasa mabondia wa timu ya mkoa wa Dar es salaam wapo kambini wakijiandaa na mashindano ya majiji yatakayoanza Kampala Uganda Aprili 2 mwaka huu
Timu hiyo ambayo ipo na makocha wazoefu inaongozwa na David Yombayomba ,Ferdnand Nyagawa mazoezi yanayofanyika kila siku Mgulani JKT, wakisaidiwa na Mazimbo Ally na Kameda Antony
Timu hiyo ina mahitaji mbalimbalio ikiwemo kambi pamoja na gharama za kupeleka timu Uganda kiasi cha shilingi  milioni 16 kwa ajili ya kwenda kwenye mashindano
hayo ambapo mpaka sasa wamejaribu kuomba misaada  sehemu mbalimbali yakiwemo makampuni  na  watu binafsi hata hivyo hakuna mafanikio yoyote hivyo tunawaomba  wadau wa mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kusaidia timu hiyo ambayo inakabiliwa na mashindano ya majiji

HIVI NDIVYO MVUA ILIVYOHARIBU MAZINGIRA JIJINI DAR

Mwavuli unaotumiwa na wafanyabiashara wadogowadogo  ukiwa umechukuliwa na maji na kutumbukia kwenye shimo eneo la stendi ya mabasi Ubungo.
         Maji yakiwa yametuama kwenye shimo stendi ya mabasi Ubungo.
Mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jana na leo imesababisha maafa kwenye baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam ambapo katika mizunguko ya  kamera yetu  imenasa  eneo la nje ya stendi ya Mkoa, Ubungo maji yakiwa yamejaa kila  pande huku wafanyabiashara wadogo wanaofanyia kazi eneo hilo, miavuli yao na vitendea kazi vikisombwa na maji huku mashimo yaliyokuwa yamechibwa katika utengenezaji wa barabara yakizidi kuporomoka.

AJABU:MCHUNGAJI WA KANISA LA KILOKOLE AZIKWA KWA NGUVU KIISLAM SOMA KISA HAPA!!

Maajabu! Mchungaji wa Kanisa la Pentecostal Spirit and Truth, Amani Rubeni Mirumbe ameushangaza ulimwengu kwa kujitabiria kifo na baadaye kufariki dunia kweli huku akiwaachia waumini na familia yake wosia wenye viashiria vya kuzikwa Kiislam, Amani linakujuza.
 
 Mwili wa mchungaji Amani Rubeni Mirumbe ukiagwa.
Kifo hicho kilijiri saa 3:12 asubuhi ya Machi 24, mwaka huu, Mabibo jijini Dar es Salaam mahali lilipo kanisa na nyumba ya mchungaji huyo na kuzikwa saa 10:21 jioni. Kwa maana hiyo, mwili huo ulikaa kwa saa saba tu.
KILICHOSABABISHA KIFO
Saa chache baada ya kifo, Amani lilifika msibani na kufanikiwa kubaini mawili matatu kuhusu kifo cha mtumishi huyo wa Mungu.
Kwa mujibu wa mmoja wa waumini wake, marehemu Mchungaji Mirumbe alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya presha lakini asubuhi ya siku ya tukio, alipoamka alimwita msaidizi wake na kumwambia siku hiyo haiwezi kupita bila yeye kukata roho.
“Ni ajabu sana, alipoamka tu alimwita msaidizi wake, akamwambia siku ya leo (Jumatatu) lazima afe ila kabla ya kuiacha dunia anataka kuacha wosia wake kwa ajili ya familia na sisi waumini,” alisema muumini mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina.
WOSIA NI HUU
Muumini huyo alisema kuwa, mchungaji huyo akiwa katika hatua za mwishomwisho kabla ya kifo, aliacha wosia kwamba, akishakata roho hatataka mwili wake uzikwe ukiwa ndani ya jeneza kama wafanyanyiwavyo Wakristo au wachungaji wengine.
 
Ndugu wa mchungaji Amani Rubeni Mirumbe wakiomboleza kwa simanzi kubwa
“Marehemu aliagiza mwili wake uwekwe kwenye sanda na hata kama ataagwa zoezi hilo lifanyike mwili ukiwa ndani ya s
anda ambayo itazungushiwa mkeka,” muumini huyo alizidi kuanika wosia huo.
KUHUSU MAITI YAKE
Katika wosia huo, Mchungaji Mirumbe aliagiza maiti yake isilale hata usiku mmoja na wala isisafirishwe kwenda kwao mkoani Mara kwa mazishi.“Alisema akitokea mtu kimbelembele na kujiamulia kuisafirisha maiti yake kwenda kuzikwa kokote nje ya Dar, basi ajue atarudi nayo atake asitake,” kilisema chanzo.

HAKUNA KULIA
Mwisho marehemu huyo hakutaka waumini wake wale familia yake kumwaga machozi kufuatia kifo chake kama njia ya kuomboleza.
 
WAUMINiWAUPOKEA MWILI
Amani liliwashuhudia waumini wa kanisa hilo wakiupokea mwili wa mchungaji wao kutoka ndani ya nyumba yake ulikokuwa umehifadhiwa baada ya kifo ukiwa umeviringishwa kwenye mkeka na kupelekwa kanisani kwa ajili ya kuombewa na kuagwa kabla ya kupelekwa makaburini.
Wakati wa kuuaga mwili, baadhi ya ndugu na waumini wachache walionekana kuvunja wosia wa mchungaji huyo ambapo walionesha wazi masikitiko yao kwa kuangua vilio licha ya kuonywa na baadhi ya viongozi.
HALI YA MAKABURINI
Mwili huo ukiwa ndani ya sanda iliyozungukwa na mkeka uliwekwa juu ya meza ndani ya kanisa lake. Baada ya zoezi hilo, ndugu na waumini waliuchukua mwili huo hadi kwenye Makaburi ya Ubungo Fishnet Industry ‘Ufi’, Shekilango jijini Dar kwa mazishi ambapo mwili uliingizwa kwenye mwanandani.
Baadhi ya ndugu na waumini walisimamia wosia kuhakikisha hakuna kisichofuatwa ambapo walisimamia zoezi la kumzika mchungaji huyo pasipo kitu chochote zaidi ya sanda tu kama alivyoagiza.
 
  Mwili wa mchungaji Amani Rubeni Mirumbe ukizikwa.
MTOTO WA MAREHEMU ANENA
Akizungumza na mwandishi wetu makaburini hapo, mtoto wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Adam Mirumbe alithibitisha utabiri wa kifo na wosia wa baba yake kwa msikitiko.
“Kweli baba aliniambia kuwa angekufa leo na alinipa wosia kuwa maiti yake isilale, isisafirishwe, watu wasilie msibani na kubwa zaidi ni kwamba azikwe bila jeneza, yaani na sanda tu kama ulivyoona. Unaweza kusema amezikwa Kiislam, lakini yeye aliamini atakuwa amezikwa kama Yesu,” alisema mtoto huyo.

KUHUSU MKE WA MAREHEMU
Adam aliongeza kuwa, wakati kifo cha baba yake kinatokea, mama yake hakuweza kuhudhuria kwa sababu alikuwa safarini kuelekea Musoma, Mara kwenye msiba wa mtoto mwingine ambapo maziko yake ilibidi yasimamishwe mpaka mwili wa mchungaji huyo uhifadhiwe kwenye nyumba yake ya milele.
 
 Ndugu na jamaa wa mchungaji Amani Rubeni Mirumbe wakiwa kwenye maziko.
KUMBE NI BABA WA MSANII WA BONGO MUVI
Mwandishi wetu aliwashuhudia wasanii wa filamu Bongo ‘Bongo Movies’, Mohammed Mwikongi ‘Frank’ na Michael Philip ‘Kojaki’ wakimtia nguvu msanii mwenzao ambaye ni mtoto mmojawapo wa mchungaji huyo ambaye kisanii anajulikana kwa jina la Mgomakufa.

KWA  NINI KIISLAM?
Baadhi ya watu waliohudhuria msiba huo walishindilia utaratibu huo kuwa ni wa imani ya Kiislam wakidai kwamba, mwili huwa haulali (labda dharura), hauzikwi ukiwa ndani ya jeneza (sanduku) na huwekwa kwenye mwanandani.
“Sijui kwa nini mchungaji aliamua kutoa wosia huo? Huenda kuna kitu alikiona ambacho kilimpa ishara kwamba, kuzikwa ndani ya jeneza na maiti yake kulala kuna mambo atayakosa mbele ya safari akhera,” alisema mwombolezaji mmoja.
MAZISHI YA KIKRISTO
Katika utaratibu wa mazishi ya Kikristo, mwili huhifadhiwa ndani ya jeneza, unaweza kulala hata siku tatu bila kuzikwa, hakuna mwanandani kwa sababu mwili unakuwa ndani ya sanduku. Maajabu! Mchungaji wa Kanisa la Pentecostal Spirit and Truth, Amani Rubeni Mirumbe ameushangaza ulimwengu kwa kujitabiria kifo na baadaye kufariki dunia kweli huku akiwaachia waumini na familia yake wosia wenye viashiria vya kuzikwa Kiislam, Amani linakujuza.
 
 Mwili wa mchungaji Amani Rubeni Mirumbe ukiagwa.
Kifo hicho kilijiri saa 3:12 asubuhi ya Machi 24, mwaka huu, Mabibo jijini Dar es Salaam mahali lilipo kanisa na nyumba ya mchungaji huyo na kuzikwa saa 10:21 jioni. Kwa maana hiyo, mwili huo ulikaa kwa saa saba tu.
KILICHOSABABISHA KIFO
Saa chache baada ya kifo, Amani lilifika msibani na kufanikiwa kubaini mawili matatu kuhusu kifo cha mtumishi huyo wa Mungu.
Kwa mujibu wa mmoja wa waumini wake, marehemu Mchungaji Mirumbe alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya presha lakini asubuhi ya siku ya tukio, alipoamka alimwita msaidizi wake na kumwambia siku hiyo haiwezi kupita bila yeye kukata roho.
“Ni ajabu sana, alipoamka tu alimwita msaidizi wake, akamwambia siku ya leo (Jumatatu) lazima afe ila kabla ya kuiacha dunia anataka kuacha wosia wake kwa ajili ya familia na sisi waumini,” alisema muumini mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina.
WOSIA NI HUU
Muumini huyo alisema kuwa, mchungaji huyo akiwa katika hatua za mwishomwisho kabla ya kifo, aliacha wosia kwamba, akishakata roho hatataka mwili wake uzikwe ukiwa ndani ya jeneza kama wafanyanyiwavyo Wakristo au wachungaji wengine.
Ndugu wa mchungaji Amani Rubeni Mirumbe wakiomboleza kwa simanzi kubwa
“Marehemu aliagiza mwili wake uwekwe kwenye sanda na hata kama ataagwa zoezi hilo lifanyike mwili ukiwa ndani ya sanda ambayo itazungushiwa mkeka,” muumini huyo alizidi kuanika wosia huo.
KUHUSU MAITI YAKE
Katika wosia huo, Mchungaji Mirumbe aliagiza maiti yake isilale hata usiku mmoja na wala isisafirishwe kwenda kwao mkoani Mara kwa mazishi.“Alisema akitokea mtu kimbelembele na kujiamulia kuisafirisha maiti yake kwenda kuzikwa kokote nje ya Dar, basi ajue atarudi nayo atake asitake,” kilisema chanzo.

HAKUNA KULIA
Mwisho marehemu huyo hakutaka waumini wake wale familia yake kumwaga machozi kufuatia kifo chake kama njia ya kuomboleza.
 
WAUMINiWAUPOKEA MWILI
Amani liliwashuhudia waumini wa kanisa hilo wakiupokea mwili wa mchungaji wao kutoka ndani ya nyumba yake ulikokuwa umehifadhiwa baada ya kifo ukiwa umeviringishwa kwenye mkeka na kupelekwa kanisani kwa ajili ya kuombewa na kuagwa kabla ya kupelekwa makaburini.
Wakati wa kuuaga mwili, baadhi ya ndugu na waumini wachache walionekana kuvunja wosia wa mchungaji huyo ambapo walionesha wazi masikitiko yao kwa kuangua vilio licha ya kuonywa na baadhi ya viongozi.
HALI YA MAKABURINI
Mwili huo ukiwa ndani ya sanda iliyozungukwa na mkeka uliwekwa juu ya meza ndani ya kanisa lake. Baada ya zoezi hilo, ndugu na waumini waliuchukua mwili huo hadi kwenye Makaburi ya Ubungo Fishnet Industry ‘Ufi’, Shekilango jijini Dar kwa mazishi ambapo mwili uliingizwa kwenye mwanandani.
Baadhi ya ndugu na waumini walisimamia wosia kuhakikisha hakuna kisichofuatwa ambapo walisimamia zoezi la kumzika mchungaji huyo pasipo kitu chochote zaidi ya sanda tu kama alivyoagiza.
 
  Mwili wa mchungaji Amani Rubeni Mirumbe ukizikwa.
MTOTO WA MAREHEMU ANENA
Akizungumza na mwandishi wetu makaburini hapo, mtoto wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Adam Mirumbe alithibitisha utabiri wa kifo na wosia wa baba yake kwa msikitiko.
“Kweli baba aliniambia kuwa angekufa leo na alinipa wosia kuwa maiti yake isilale, isisafirishwe, watu wasilie msibani na kubwa zaidi ni kwamba azikwe bila jeneza, yaani na sanda tu kama ulivyoona. Unaweza kusema amezikwa Kiislam, lakini yeye aliamini atakuwa amezikwa kama Yesu,” alisema mtoto huyo.

KUHUSU MKE WA MAREHEMU
Adam aliongeza kuwa, wakati kifo cha baba yake kinatokea, mama yake hakuweza kuhudhuria kwa sababu alikuwa safarini kuelekea Musoma, Mara kwenye msiba wa mtoto mwingine ambapo maziko yake ilibidi yasimamishwe mpaka mwili wa mchungaji huyo uhifadhiwe kwenye nyumba yake ya milele.
 
 Ndugu na jamaa wa mchungaji Amani Rubeni Mirumbe wakiwa kwenye maziko.
KUMBE NI BABA WA MSANII WA BONGO MUVI
Mwandishi wetu aliwashuhudia wasanii wa filamu Bongo ‘Bongo Movies’, Mohammed Mwikongi ‘Frank’ na Michael Philip ‘Kojaki’ wakimtia nguvu msanii mwenzao ambaye ni mtoto mmojawapo wa mchungaji huyo ambaye kisanii anajulikana kwa jina la Mgomakufa.

KWA  NINI KIISLAM?
Baadhi ya watu waliohudhuria msiba huo walishindilia utaratibu huo kuwa ni wa imani ya Kiislam wakidai kwamba, mwili huwa haulali (labda dharura), hauzikwi ukiwa ndani ya jeneza (sanduku) na huwekwa kwenye mwanandani.
“Sijui kwa nini mchungaji aliamua kutoa wosia huo? Huenda kuna kitu alikiona ambacho kilimpa ishara kwamba, kuzikwa ndani ya jeneza na maiti yake kulala kuna mambo atayakosa mbele ya safari akhera,” alisema mwombolezaji mmoja.
MAZISHI YA KIKRISTO
Katika utaratibu wa mazishi ya Kikristo, mwili huhifadhiwa ndani ya jeneza, unaweza kulala hata siku tatu bila kuzikwa, hakuna mwanandani kwa sababu mwili unakuwa ndani ya sanduku.

Tuesday, February 4, 2014

HICHI NDICHO ALICHOKISEMA RAISI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI ARUSHA BAADA YA KUJIUZULU

Raisi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha(AJTC) akitangaza kujiuzulu nafasi ya uraisi

Raisi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji bwana George Silange aliyechaguliwa kwa ushindi mkubwa na wanafunzi wa chuo hicho katika uchaguzi uliofanyika baada aliyekuwa........