AJTC NEWS

Thursday, February 7, 2013

SERIKALI YATAKIWA KUONGEZA WAWEKEZAJI ILI KUTATUA TATIZO LA AJIRA



Wafanya biashara wa madini mkoani Arusha  wameiomba serikali kuongeza wawekezaji il kutatua tatizo la ajira kwa vijana

Akizungumza na ajtc redio kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake bi careen saitoti ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya B&BGems amesema  biashara ya madini inaweza kuinua vijana endapo itawezeshwa

Pamoja hayo ameendelea kusema endapo serikali itaanda soko bora nchini itaweza kuinua sekta hiyo ya madini ili kuzuia ubadhilifu wa madini       Tanzania akitolea mfano kenya kuweka nembo ya nchi yao kwenye madini  ya tanzanite ili kuonekana wao ndio wazalishaji wakukk wa madini hayo ikiwa tanzania ndio nchi ya pekee inayozalisha madini hayo

Hata hivyo ameishauri serikali  kuwa kuwepo  na dhamana  ya uwekezaji,kuanda soko bora  la ndani na nje ya nchi,vilevile wawekezaji walete vifaa vya kukatia madini nchini il vijana wapate ajira

Amemalizia kwa kuishauri serikali iangalie upya utoaji wa leseni na vibali vya uhimbaji wa madini kwa wageni ili waweze kufanya biashara za madini kwa manufaa ya watanzania.

No comments:

Post a Comment