AJTC NEWS

Tuesday, January 15, 2013

RAIA WA AFRIKA KUSINI WASHANGAZWA NA UBAKAKAJI ULIOKITHILI NCHINI HUMO


Raia wa Afrika Kusini wanashangazwa na ubakaji

 
Msichana mmoja alibakwa katika eneo hilo tarehe 2 Januari
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa bado anaishi katika chumba kimoja katika mtaa wa mabanda wa Soweti wakati polisi walipokuja kumkamata siku chache kabla ya mkesha wa siku kuu ya mwaka mpya.
Kwa mujibu wa mashahidi kadhaa, mtu huyo alikuwa amembaka msichana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na saba katika baa moja, na alihisi kuwa kitendo hicho ni cha kawaida na hivyo hakujaribu kutoroka.
Hamna hata mtu mmoja katika baa hiyo, mbali na msichana huyo alifikiria kupasha polisi habari kuhusiana na tukio hilo.
Wakati ambapo taifa la India, linachunguza sheria za nchi hiyo kufuatia tukio la ubakaji, Afrika Kusini inaonekana kuwa imezembea.
Serikali ya nchi hiyo imeonekana kutojali yale yanayotendeka licha ya takwimu kubainisha viwango vya ubakaji nchini humo viko juu hata kuliko taifa la India.

Friday, January 11, 2013

Watu 11 zaidi wauawa Tana River


Takriban watu kumi na mmoja wameuawa katika mapigano zaidi katika eneo la Tana River Kusini Mashariki mwa Kenya.
Ripoti zinasema miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo lililotokea alfajiri ya siku ya Alhamisi ni watoto watano.
Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa shambulio hilo ni la kulipisa kisasi mauaji yaliyotokea katika eneo hilo usiku wa kuamkoa siku ya Jumatano dhidi ya watu wa jamii wa Orma.
Watu wengine tisa waliuawa siku ya Jumatano pale wapiganaji wa Pokomo walipoishambulia kijiji kimoja cha watu wa Orma na kutetekeza nyumba na kuiba mifugo.

Kulipisa kisasi

Wengi wa waliojeruhiwa wakati wa shambulio hilo ni watu wa kabila la Orma.
Walionusurika shambulio hilo wanaendelea kutibiwa katika hospitali kadhaa kutokana na majeraha ya risasi, panga na moto.
Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kuwa watu waliokuwa wamejihami kwa silaha walivamia kijiji cha watu wa Orma na kuwaua watu sita.
Shambulio hilo katika kijiji cha Kibusi linajiri siku moja baada ya shambulio lingine lililotokea jana katika kijiji jirani ambako watu wengine sita waliuawa.
Kwa mujibu wa shirika hilo, vijiji hivyo viko umbali wa kilomita ishirini na kuna kituo kimoja cha polisi katikati.
Zaidi ya mia moja waliuawa katika mashambulio kama hayo mwaka uliopita na hali ya usalama katika eneo hilo umeimarishwa.
Watu wa jamii hizo mbili walikabiliana mwezi Agosti mwaka uliopita baada ya watu wa jamii ya Ormo kushutumiwa kulisha mifugo wao katika mashamba ya watu wa jamii ya Pokomo.

Wabunge Kenya wajizawadi mamilioni ya dola

Wabunge nchini Kenya wamejizawadia dola 107,000 kama marupurupu katika mojawpao ya vikao vyao vya mwisho vya bunge hilo kabla ya uchaguzi mkuu kufayika mwezi Machi.
Kila mbunge ataweza kupata mlinzi wa maisha, pasi ya kidiplomasia na kupata huduma za juu zaidi katika viwanja vye ndege kote duniani. Haya ndiyo mapendekezo yaliyo katika mswaada waliopiitisha ukisubiri kuidhinishwa na rais MwaiKibaki.
Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wabunge wanaopokea mishahara ya juu zaidi barani Afrika kila mmoja akipata dola elfu kumi na tatu kila mwezi.Ni mara ya pili wabunge wamepitisha mswaada huu wa kujizawadia mwishoni mwa vikao vyao vyabunge . Rais Mwai Kibaki alitupilia mbali mswaada wa kwanza kama huu ambao ulizua ghadhabu miongoni mwa wananchi.
Lakini mshahara wa mkenya wa kawaida ni takriban dola 1,700 kila mwezi.
Mswaada huu, ulipitishwa siku ya Jumatano na wabunge chini ya thelathini waliokuwa bungeni. Walikarabati bunge lao kwa kutumia dola milioni kumi na mbili kulingana na stakabadhi za bunge zilizotolewa hapo jana.
Malipo haya ni sawa na yale yaliyokuwepo katika mswaada walioupitisha mwezi Oktoba, lakini wakati huu wabunge hao pia wamependekeza marupurupu kwa rais ambaye atalipwa dola laki tatu sawa na makamu wa rais na waziri mkuu.
Alipotupilia mbali mswaada wa kwanza , Rais Kibaki lisema kuwa haiwezekani kwa wabunge kulipwa mamilioni ya dola wakati uchumi ungali umedumaa.
Tume ya kushughulikia mishahara ya wafanyakazi wa umme, iliambia wakenya kuwa hakuna uhakika ikiwa hatua yao inakuika katiba.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yameelezea kukerwa sana na hatua ya wabunge. Tayari waziri mkuu Raila Odinga amepinga mswaada huo akisema kuwa ni kama uhalifu dhidi ya wakenya na kwamba anashauriana na rais Mwai Kibaki kuhusu hatua itakayokuwa sawa kwa wakenya.


Bunge jipya lililokarabatiwa kwa zaidi ya dola milioni kumi




Ayew aachwa nje ya kikosi cha Ghana


Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Ghana Kwesi Appiah, amemuondoa Andre 'Dede' Ayew katika kikosi chake kitakacho shiriki katika michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika.
Ayew, alikosa kufika kambini Abu Dhab kutokana na jeraha la paja, ambalo bado halijathibitishwa na madaktari wa timu hiyo.
Mcheza kiungo huyo aliruhusiwa na klabu yake ya Ufaransa ya Marseille, ili ajiunge na timu hiyo ya taifa ya Ghana, kufuatia ombi lililowasilishwa kwa klabu hiyo na shirikisho la mchezo huo nchini Ghana.
'' Nimeamua kumuacha nje ya kikosi changu kitakacho elekea Afrika Kusini'' Alisema Appiah.

Sheria za FIFA

Andre Ayew akisherehekea bao lake
Chini ya sheria za FIFA, vilabu vya soka vinapaswa kuwaruhusu wachezaji siku ya Jumamosi, wiki mbili kabla ya kuanza kwa fainali hizo za Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini.
Vilabu pia ni shartiw aruhusu wachezaji waliojeruhiwa kuchunguzwa na madaktari wa timu zao za taifa.
''Andre hakujitokeza, licha ya kuwa tayari alikuwa amepewa idhini na klabu yake na pia kukabithiwa tikiti ya ndege ya shirikisho la mchezo wa soka la Ghana, ili asafiri kutoka Ufaransa hadi kambini'' Kocha huyo aliongeza.
Mchezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ghana
Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa hakufika kambini na kusema kwamba hakuwa amemaliza matibabu aliyokuwa akipewa na daktari wake ili afike kambini siku ya Jumatano, tarehe 9 mwezi huu.
''Mchezaji huyo aliamriwa kufika kambini siku ya Jumatatu kwa kuwas siku ya Jumatano ndio siku ya mwisho kwa nchi mbali mbali kuwasilisha majina ya wachezaji wake kwa shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika CAF.
Appiah kwa sasa ana kikosi cha wachezaji 25 na ni sharti apunguze kikosi hicho kabla ya siku ya Jumatano, wakati atakapotaja rasmi kikosi kitakacho akilisha Ghana kwenye faianli hizo.
Ghana inaanza kampeini yake ya fainali hizo za Afrika tarehe 20 Januari dhidi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kabla ya kucheza na Mali na Niger katika kundi B.

Nigeria won the African Cup 2013?


Wacheza kamali wanataka kucheza karata zao vizuri kuhusu kinyang'anyiro cha ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013. Wacheza kamali hao wataelekeza karata yao katika timu ya Nigeria wakiipa nafasi ya kuwa katika timu tatu bora za juu.

Timu ya Nigeria, The Super Eagles, imeshiriki mara 16 katika mashindano ya kombe hilo na kushinda mara mbili, ikishika nafasi ya pili mara nne na mara saba katika nafasi ya tatu, ikiwa ni rekodi ya kujivunia katika kipindi cha miaka 50.
Ni katika mwaka 1963 na 1982 (ikiishia raundi ya kwanza) na 2008 (robo fainali) Eagles wakishindwa kutwaa medali na wanaonekana wamejipanga angalau kuingia nane bora katika fainali za mwaka 2013 nchini Afrika Kusini baada ya kupangwa katika kundi C pamoja na timu za Burkina Faso, Ethiopia na Zambia.
Kocha wa timu ya Nigeria, Stephen Keshi
Timu zinazoshika nafasi ya kwanza na ya pili katika makundi, husonga mbele na kuingia robo fainali. Nigeria na mabingwa watetezi Zambia wanapewa nafasi ya kusonga mbele. Kwa mshangao timu ya Nigeria, The Super Eagles, walishindwa kufuzu katika fainali za mwaka 2012zilizoandaliwa kwa pamoja kati ya Gabon na Equatorial Guinea na ilimgharimu kocha wake Samon Siasia wakati aliposhindwa kuongezewa mkataba.
Kocha wa sasa Stephen 'Big Boss' Keshi, kocha asiye na mzaha ambaye alikuwa katika kikosi cha wachezaji wa Nigeria walioishinda Zambia kwa kuilaza magoli 2-1 katika fainali zilizofanyika Tunisia, miaka 19 iliyopita. Alikuwa mchezaji kiungo imara ambaye aliongoza kwa mfano na alitumia wiki chache zilizopita kufanya mazoezi katika kambi nchini Ureno akijaribu kujenga moyo wa ushindi kwa timu yake ya Super Eagles.
Obi Mikel akidhibiti mpira
"Nataka wachezaji wenye njaa ya kusaka ushindi, wenye kujitolea na ambao wanajivunia kuchezea timu ya taifa ya Nigeria," amesisitiza kocha huyo ambaye alipambana na Togo na Mali bila kufuzu hatua ya kwanza katika mashindano yaliyotangulia ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
"Ni vizuri kuona wachezaji wakifanya jitihada kuwania namba katika kikosi changu cha kwanza. Ushindani huo unanipa changamoto nzuri. Hakuna mwenye namba ya kudumu katika timu-- ni lazima wapiganie na pia wapiganie kuhifadhi namba wanayopataKocha wa Mlinzi wa kati na nahodha wa Super Eagles, Joseph Yobo, analeta changamoto sawa katika rekodi ya mchezaji bora wa zamani wa mwaka wa Afrika Nwankwo Kanu kwa kucheza katika fainali sita za Kombe la Afrika.
"Kushinda kombe si kazi rahis lakini naahidi kutafanya kwa uwezo wetu wote kufikia lengo hilo. Nawaomba Wanaigeria kutuombea na kuwa na imani na timu hii,"anasema mchezaji huyo kiungo wa zamani wa Everton ambaye kwa sasa anacheza soka nchini Uturuki.
"Tunasafiri kwenda Afrika Kusini tayari kupeperusha bendera ya taifa letu na hatutachoka hadi tutakapotimiza lengo letu. Bahati nzuri tuna kikosi kizuri cha wakufunzi ambacho kinatufahamu vizuri na nina uhakika wachezaji wako tayari kwa hilo.

MANYARA Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja Rashid aliyekuwa mkandarasi wilayani kiteto mkoani manyara amefariki dunia mwishoni mwa wiki hii baada ya kujinyonga hadi kufa kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.

MANYARA

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja Rashid aliyekuwa mkandarasi wilayani kiteto mkoani manyara amefariki dunia mwishoni mwa wiki hii baada ya kujinyonga hadi kufa kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.

Kabla ya kifo hicho marehemu alitodfautiana na mkewe aliyekuwa akifanya kazi ya ualimu shule ya msingi nameloki kata ya katembo hapo aliondoka shuleni na kumuacha marehemu mjini kibaya katika shughuli zake .

Taarifa za polisi zinasema kuwa marehemu alimfuata mke wake kijiji cha namiloki kata katembo siku moja baada ya ugomvi ambapo hapo alianza upya ugomvi huo ndipo mke wake kuanza kuomba msaada kwa afia mtendaji wa kijiji hicho.

Wakati akiwa anarejea kwake akiwa na mtendaji wa kijiji walimkuta mume wake huyo amening'inia juu ya paa ambapo hapo waliwahi kukata kamba aliyotumia kujinyonga na akadondoka akiwa hai hatimaye kukimbizwa hospitali ya wilaya ya kiteto kwa matibabu.

Wakiwa njiani kuelekea hospitali alifariki dunia kwa kile kinachodaiwa baadhi ya mishipa ya shingo ilikatika na mwili wa marhemu umeshahifadhiwa katika hospitali ya kiteto kusafirishwa kwenda kwa mazishi .

  

KILIMANJARO Vitendo vya uchawi na ushirikina vimeshamiri katika kijiji cha kitandu kata ya kibosho mkoani kilimanjaro

KILIMANJARO
Vitendo vya uchawi na ushirikina vimeshamiri katika kijiji cha kitandu kata ya kibosho mkoani kilimanjaro

Haya yamesemwa na diwani wa kata hiyo bwana moris kimati amesema uchawi umekuwa kikwazo cha maendeleo katika kijij hicho

Watu wengi wa kijiji hicho wamepoteza maisha kwa ajili ya uchawi hali inayochangi wanakijiji hao kushindwa kufanya kitu chochote cha maendeleo

Amesema wanakijiji hao wameogopa kujenga hata nyumba nzuri katika viwanja vyao kwa kuhofia kupoteza maisha

Wakazi wa kijiji hicho wamelazimika kuhama katika maeneo yao na kutafuta maeneo mengine hivyo wameshauliwa kuachana na vitendo hivyo ili waweze kupata maendeleo katika kijiji chao

Thursday, January 10, 2013

JE UNAFAHAMU KABILA LA WAHAYA NA TAMADUNI ZAO

        JE UNAFAHAMU KABILA LA WAHAYA NA TAMADUNI ZAO

Kabila la wahaya ni kabila lilopo mkoani Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania. kabila hili lipo kandokando mwa ziwa Victoria lugha yao ni kihaya kabila hili ndo kubwa mkoani Kagera kutokana na sensa iliyofanyika siku za hivi karibuni.

Yupo mmoja ambae ni mwanamziki wa kihaya ambaye katika nyimbo zake zina vionjo vingi vya kabila la kihaya japo kwa sasa ameporomoka kwa muda naye ni SAIDA KAROLI.
       
                              kwa kujua zaidi tembelea blog hii ili uweze kujua mengi zaidi kuhusiana na wahaya.

MAKALA YA UJASIRIAMALI

MAKALA YA UJASIRIAMALI

Katika ulimwengu wa sasa kila kitu ni kujifunza tu mwenyewe ili uweze kuyamudu maisha ya sasa na ya baadae tukizungumzia swala la maisha ni lazima tugusie ujasiriamali

Hata hivyo ujasiriamali unaweza kujitokeza katika taswira tofauti lakini kwa lengo moja tu ili kuleta maendeleo ndani ya jamii yetu. iwapo kila mmoja kwa nafasi yake atajitokeza na kuweza kujishughulisha katika maswala mbalimbali ya kujipatia kipato kwa ajili ya kumudu au kukidhi mahitaji yake kimaisha.

Lakini kikubwa zaidi kabla ya kuendelea mbele ni lazima tujiulize swali kuwa ujasiriamali ni nini? kwani swala hili la ujasiriamali huwatatiza wengi hasa wale ambao hawajapata elimu hususani ile inayo jihusisha na ujasiriamali ama kwa lugha ya kizungu huitwa (ITERPRINUERSHIP) ambapo hii imetokana na lugha ya wenzetu wafaransa.

Ujasiriamali ni ile hali ya kuwa na ujasiri wa kuanzisha biashara kwa ujasiri bila kuogopa kitu chochote ama mtu yeyote kuwa atakuonaje ama atakuchukuliaje kwa njia yeyote ama mtazamo wowote.

 Sifa ya ujasiriamali haichagui kuwa wewe unataka kuanzisha biashara gani yaweza ikawa ni biashara ya ufugaji,kilimo, ama biashara yeyote ile ila lengo liwe ni kukidhi mahitaji yako au kujipatia kipato ambacho kitakutoa kutoka kwenye kipato kidogo mpaka kikubwa (Fanya fedha zako  ziendelee kuwa za kwako)


Ukiwa kama mjasiriamali kabla ya kuanzisha biashara kuna mambo makuu ya kuzingatia ikiwa ni pamoja kuwa na wazo ndipo mtaji ufuate. wazo lenyewe linatakiwa lihusishe biashara unayotaka kuifanya au kuanzisha kwa wakati huo.ukishajua ni biashara gani unataka kuanzisha  ni lazima ufanye utafiti ili uweze kujua hiyo biashara inagharimu kiasi gani cha fedha

Mtaji ni kiwango cha fedha ambacho wewe mjasiriamali unakiandaa kwa ajili ya kuendeshea biashara yako nakumbuka kuwa mtaji huo unaweza kuwa mdogo au mkubwa hii inatokana na uwezo wa mtu mwenyewe aliopanga kwa ajili ya hiyo biashara

Siku zote mtaji ndiyo jicho la biashara yako kwani unapoanzisha biashara unatakiwa isiporomoke au kuisha kabisa kwa maana hiyo mtaji hauna budi kulindwa kwenye biashara yoyote kubwa ama ndogo kwa hali yoyote ile mtaji ni lazima ulindwe na mjasiriamali ili lengo lake au ndoto zake ziweze kutimia na kuwa mjasiriamali mkubwa kwa kupitia uboreshaji wa biashara yake

Na katika biashara kuna makundi mengi ya biashara,kwanza kuna biashara ya mtu mmoja mmoja na kuna biashara ya makundi yaani [PATNERSHIP BUSINESS] ambapo ile ya mtu mmoja mmoja kwa na nafasi yake huitwa [PRIVATE BUSINESS] pamoja na nyingine nyingi kama limited company business

Makundi yote haya ya biashara huitaji mtaji kwa ajili ya kuendeshea biashara husika na kugharimu kiasi cha fedha kutokana ukubwa wa biaashara husika si haya tu bali makundi haya hutofautiana njia za umiliki na uendeshaji wa biashara ila yotee yanalengo moja tu za kuingiza faida na si vinginevyo

 
  MAKALA HII ITAENDELEA...................

Wednesday, January 9, 2013

Wajasiriamali wadogo ndani ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha wameusifu uongozi wa chuo hicho kwa kutoa mafunzo ya ujaririamali yanayowawezesha kujipatia mahitaji muhimu pindi wawapo masomoni

ARUSHA

Wajasiriamali wadogo ndani ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha wameusifu uongozi wa chuo hicho kwa kutoa mafunzo ya ujaririamali yanayowawezesha  kujipatia mahitaji muhimu pindi wawapo masomoni

Akizungumza mmoja wa wajasiriamali hao bi.Frola ambae anajishughulisha na kupika chakula wakati wa jioni amesema kuwa  pindi alipopata mafunzo hayo na kuyafanyia kazi ameweza kujikimu katika mahitaji madogo ambayo ni ya lazima

Ameendelea kwa kusema kupitia mafunzo hayo ameweza kujifunza jinsi ya kutunza na kuongeza fedha  ili kuweza kupata faida ambayo inamuwezesha kuendeleza shughuli hiyo

Pia mmoja wa wawatumiaji wa chakula hicho ndani ya chuo hicho bwana Azizi Munuka amesema anafurahia huduma hiyo kwani ipo karibu na ina gharama nafuu tofauti na huduma zinazopatikana nje ya chuo

Amemalizia kwa kusema anashukuru uongozi wa chuo hicho mbali na mafunzo ya uandishi wa habari na utangazaji kuwepo kwa semina mbalimbali ikiwepo ya ujasiriamali ambazo zinapanua upeo wa kutafuta fedha na kuachana na kuwategemea wazazi zaidi.

Rais wa serikali ya wanafunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha AJTC amewaonya wanafunzi kutochelewa chuo pindi wanapofungua chuo

ARUSHA

Rais wa serikali ya wanafunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha AJTC amewaonya wanafunzi kutochelewa chuo pindi wanapofungua chuo 

Hayo yamesemwa jana na rais  wa chuo hicho bwana david patric pindi alipokuwa akitoa adhabu kwa baadhi ya wanafunzi katika chuo hicho

Kuwepo na sababu za msingi pindi mwanafunzi anapochelewa kufika chuoni amesema hayo bwana Patric

Hata hivyo katibu wa chuo hicho bwana Michael Mosses amefanya juhudi ya kuwatafuta wale wote waliochelewa kufika chuoni na kuhakikisha wamepata adhabu ili kukomesha kitendo hicho cha uchelewaji chuoni hapo

Pia mmoja wa wanafunzi anaehusika katika uchelewaji huo ambae hakutaka jina lake lifahamike amesema kuwa uchelewaji wa wanafunzi ni kutokana na kutopewa mahitaji muhimu na wazazi wao kwa wakati husika

Mwanafunzi huyo amemalizia kwa kusema kuwa pamoja na adhabu zinazotolewa kutafutwe njia mbadala ili wazazi waweze kutoa mahitaji yao kwa wakati husika.