AJTC NEWS

Thursday, February 7, 2013

UCHAFUZI WA MAZINGIRA

kutokuwepo kwa utaratibu mzuri wa ukusanyaji taka katika eneo la mji mpya kwa morombo jijini arusha unaweza kupelekea kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko

Akizungumza na ajtc radio Bi Eunicee Julius ambaye ni mmoja kati ya waathirika wa tatizo hilo amsema kuwa uchsfu huo umekuwa ni kero kutokana  na utupaji taka ovyo na kusababisha kuwpo kwa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu,kuhara na kutapika

Aidha Bi Eunice ameendelea kusema uchafuzi wa mazingira ni hatari hasa kwa wakazi waishio katika eneo hilo kutokana naile hali ya kutupa taka ovyo bila kujali afya zao

Pamoja na hayo Bi Eunice ameongezea kwa kusema kuwepo kwa utaratibu mzuri wa utupaji taka ili kuweza kuepuka magonjwa yanayozuilika kwa wakazi wa eneo hilo

Hata hivyo mwenyekiti wa eneo hilo Bw Lucas John amesema tatizo hilo liko mbioni kutatuliwa hivyo amewaomba wananchi kuwa wavumilivu ili kuwekwe utaratibu mzuri wa utupaji taka hizo

No comments:

Post a Comment