Raia wa Afrika Kusini wanashangazwa na ubakaji

Msichana mmoja alibakwa katika eneo hilo tarehe 2 Januari
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa bado anaishi katika chumba kimoja katika mtaa wa mabanda wa Soweti wakati polisi walipokuja kumkamata siku chache kabla ya mkesha wa siku kuu ya mwaka mpya.
Kwa mujibu wa mashahidi kadhaa, mtu huyo alikuwa amembaka msichana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na saba katika baa moja, na alihisi kuwa kitendo hicho ni cha kawaida na hivyo hakujaribu kutoroka.
Hamna hata mtu mmoja katika baa hiyo, mbali na msichana huyo alifikiria kupasha polisi habari kuhusiana na tukio hilo.
Wakati ambapo taifa la India, linachunguza sheria za nchi hiyo kufuatia tukio la ubakaji, Afrika Kusini inaonekana kuwa imezembea.
Serikali ya nchi hiyo imeonekana kutojali yale yanayotendeka licha ya takwimu kubainisha viwango vya ubakaji nchini humo viko juu hata kuliko taifa la India.
No comments:
Post a Comment