AJTC NEWS

Sunday, August 25, 2013

  • Ajtc stars yazidi kufanya vibaya katika mechi za kujipima nguvu
  • Matumaini ya kuitetea ubingwa wa kombe la media bonaza bado ni ndoto

Kikosi cha A.J.T.C STARS

Timu ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha(AJTC STARS) bado ipo katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa media bonanza, lakini timu hiyo bado haifanyi vizuri katika mechi zake za kiurafiki.

Kwani timu hiyo ilifungwa magoli 2 kwa..................
1 na timu ya maafande wa fid force katika mechi ya kirafiki iliyochezwa siku ya ijumaa.

Mechi hiyo ya kirafiki ambayo ilingurumishwa katika dimba la fid force lililopo kwa murombo arusha ilikuwa na lengo la kuipima nguvu timu ya ajtc stars lakini walijikuta wakiangukia pua kwa maafande hao wa fid force.
Ni Ajtc stars ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la timu pinzani mnamo kipindi cha kwanza ambapo jeremiah aliiandikia ajtc stars bao la kwanza baada ya goli kipa kutema mpira ndani ya eneo la hatari na jeremia kuupachika bao wavuni, na hadi refarii anapuliza kipenga kuashiri dakika 45 za mwanzo zimekwisha ajtc stars walikuwa kifua mbele kwa bao 1.

Lakini kibao kiligeuka katika kipindi cha pili kwani mnamo dakika ya
 60 maafande wa fidforce walisawazisha bao hilo kwa kupitia mchezaji wao nambari 10, lakini jahazi la ajtc stars ilizidi kuzamishwa na maafande hao kwani mnamo dakika ya 80 ya mchezo mchezaji yuleyule aliipachikia timu yake bao la pili na la mwisho, na hadi refarii anapuliza kipenga cha mwisho ajtc stars walikuwa wamecharazwa mabao  2-1.

Mbali na hayo timu ya ajtc stars baado ni mabingwa watetezi wa kombe la media bonanza.lakini matumaini ya kutetea ubingwa huo bado ni mdogo sana, kwani timu hiyo inakumbwa na uhaba wa vifaa vya kuchezea pamoja na kufanyia mazoezi kama vile mpira, jezi pamoja na dawa za huduma ya kwanza pindi mchezaji anapoumia.

Timu hiyo bado haina matumaini kama itaweza kutetea ubingwa wake wa media bonanza ambayo inatarajiwa kutimua vumbi september 8 mwaka huu kwa kuzishirikisha timu mbalimbali kutoka ukanda wa kaskazini na itachezwa katika uwanja wa general tayre iliopo maeneo ya njiro jijini arusha

No comments:

Post a Comment