MANYARA
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja Rashid aliyekuwa mkandarasi wilayani kiteto mkoani manyara amefariki dunia mwishoni mwa wiki hii baada ya kujinyonga hadi kufa kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.
Kabla ya kifo hicho marehemu alitodfautiana na mkewe aliyekuwa akifanya kazi ya ualimu shule ya msingi nameloki kata ya katembo hapo aliondoka shuleni na kumuacha marehemu mjini kibaya katika shughuli zake .
Taarifa za polisi zinasema kuwa marehemu alimfuata mke wake kijiji cha namiloki kata katembo siku moja baada ya ugomvi ambapo hapo alianza upya ugomvi huo ndipo mke wake kuanza kuomba msaada kwa afia mtendaji wa kijiji hicho.
Wakati akiwa anarejea kwake akiwa na mtendaji wa kijiji walimkuta mume wake huyo amening'inia juu ya paa ambapo hapo waliwahi kukata kamba aliyotumia kujinyonga na akadondoka akiwa hai hatimaye kukimbizwa hospitali ya wilaya ya kiteto kwa matibabu.
Wakiwa njiani kuelekea hospitali alifariki dunia kwa kile kinachodaiwa baadhi ya mishipa ya shingo ilikatika na mwili wa marhemu umeshahifadhiwa katika hospitali ya kiteto kusafirishwa kwenda kwa mazishi .
No comments:
Post a Comment