ARUSHA
Wajasiriamali wadogo ndani ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha wameusifu uongozi wa chuo hicho kwa kutoa mafunzo ya ujaririamali yanayowawezesha kujipatia mahitaji muhimu pindi wawapo masomoni
Akizungumza mmoja wa wajasiriamali hao bi.Frola ambae anajishughulisha na kupika chakula wakati wa jioni amesema kuwa pindi alipopata mafunzo hayo na kuyafanyia kazi ameweza kujikimu katika mahitaji madogo ambayo ni ya lazima
Ameendelea kwa kusema kupitia mafunzo hayo ameweza kujifunza jinsi ya kutunza na kuongeza fedha ili kuweza kupata faida ambayo inamuwezesha kuendeleza shughuli hiyo
Pia mmoja wa wawatumiaji wa chakula hicho ndani ya chuo hicho bwana Azizi Munuka amesema anafurahia huduma hiyo kwani ipo karibu na ina gharama nafuu tofauti na huduma zinazopatikana nje ya chuo
Amemalizia kwa kusema anashukuru uongozi wa chuo hicho mbali na mafunzo ya uandishi wa habari na utangazaji kuwepo kwa semina mbalimbali ikiwepo ya ujasiriamali ambazo zinapanua upeo wa kutafuta fedha na kuachana na kuwategemea wazazi zaidi.
No comments:
Post a Comment